Amos 5:15-16


15 aYachukieni maovu, yapendeni mema;
dumisheni haki mahakamani.
Yamkini Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote
atawahurumia mabaki ya Yusufu.

16 bKwa hiyo hili ndilo Bwana, Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote, asemalo: “Kutakuwepo maombolezo katika barabara zote
na vilio vya uchungu katika njia kuu zote.
Wakulima wataitwa kuja kulia,
na waombolezaji waje kuomboleza.
Copyright information for SwhKC